August 14, 2020

Kinaya cha Mapenzi: Siku za Mwizi

4982879898940869063

Na Steve Njuguna

Simon alitizama saa yake ya mkononi,ilikuwa aina ya Seiko kutoka Japan. Ilikuwa saa tatu asubuhi na bado alikuwa hajaenda shule. Aliingia mvunguni mwa kitanda, alipoficha redio yake ndogo. Akaskiza muziki aina ya reggae huku akitingiza kichwa chake kwa utamu wa muziki. Akaangalia simu yake na kuona arafa kutoka kwa baba yake. Arafa ile ilinuia kumjulia hali na pia kumfahamisha jinsi mambo yalivyo kuwa nyumbani. Lakini Simon alipoiona kuwa watu nyumbani aliifuta mara moja.

Mtirirko wa mawazo ulimjia lakini wazo moja likawa ndilo kuu. ‘Njaa, mbona kunikera?’, alifikiria.

Aliufungua kabati iliyokuwa kando na kitanda chake na kukagua shillingi kadhaa zilizojisatiri humo. Hela zilimtizama kana kwamba zina huzuni. Akachukua shilling ishirini za kununulia chai na kuelekea mlangoni lakini akasimama kwa ghafla aliposikia sauti ya mtu nje.

“Simon! Ni mimi Beka na nataka pesa zangu, miezi miwili hujalipa kodi jamani!”

Simon alinyamelea polpople na kujificha mvunguni mwa kitanda ili asionekane.

“Naskia redio ndani ya hiyo nyumba , najua uko ndani na utatoka tu!”

Simon akatoka mvunguni aliposikia Beka akiondoka. Akaanza kuwaza jinsi ataweza kuhepa Beka na kuondoka kule kwake. Wazo lake lilikatizwa na mlio wa simu yake .

“Hello, sasa beib,” sauti iliyokuwa na mnato wa kike ilisabahi

“Poa sana sweetie,” alijibu huku akitabasamu.

“Si leo unanipeleka movie?” sauti iliuliza kwa upole.

“Of course dear, lazima,” alisema huku tabasamu ikiisha pole pole.

“Aaaw love you beib, see you,” sauti ilijibu kwa furaha.

Simon alikata simu na kujishika kichwa kana kwamba kingeanguka. Alijua pesa hangepata kutoka nyumbani kwani walikuwa wamemtumia pesa za kodi juzi. Alikuwa pia amekopa wenzake hadi urafiki ukaisha. Shida hizi zote, ili tu kumfurahisha Mercy, kidosho fulani ambaye walipatana kule shule, na Simon akapendezwa na urembo wake. Hakuna ambacho Simon hangekifanya kumfurahisha msichana yule.

Na wenzake walipomuonya, alidai eti wana wivu.

Alivalia nguo na kujipaka manukato huku akivaa viatu aina ya ‘Supra’. Akatoka kwa nyumba na kufunga mlango pole pole ili Beka asije aanze kumdai kodi. Akaelekea kwenye kituo cha basi na kungoja matatu huku akifikiria atakapotoa shilling elfu tatu za kumpeleka Mercy kutazama sinema na kumnunulia chakula. Baada ya dakika kadhaa alipata matatu na kuelekea jijini huku mawazo yakimtatiza.

Alipofika jijini Nairobi, alishuka kutoka kwa matatu na kuelekea Gikomba, kumwona rafiki abaye labda angeweza kumfaa.

Akiendelea kutembea akamwona mwanamke mmoja mbele yake akitembea na wasiwasi. Kwa haraka zake aliangusha kibeti chake bila kujua. Simon kutazama kile kibeti aliona maelfu ndani. Aliona kuwa labda ni Mungu amemtumia suluhisho kwa shida zake. Alitazama nyuma ili kuona kama kuna mtu mwingine aliyekuwa amekiona kile kibeti. Alipotosheka kuwa hakuna mtu aliyekuwa amekiona kibeti kile aliinama kwa utaratibu na kukichukua kisha akaanza kutembea kwa kasi.

Ghafla akasikia mlio mkali.

‘Wuuuuiiii, Mwiziiiiiii!!!’

Kuangalia nyuma akaona watu wengi wakianza kumkimbiza na akaanza kukimbia. Hatimaye watu walimzidi kasi na kumbwaga chini ambapo wakamzidi nguvu kwa mangumi na mateke.

‘Achomweee! Achomwee!” watu walisema huku wakitafuta gurudumu la gari na petrol ili kumchoma. Kama siku za mwizi zilikuwa arobaini, mbona yeye kapatikana siku ya kwanza?

Aliitizama hatima yake lakini maulana akasikia kilio chake. Polisi waliwasili na kumwokoa kutokana na umati huu na kumpeleka kwenye kituo cha polisi. Siku iliyo fuata aliwasilishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha miaka nne. Huko mahakamani aliwaona wazazai wake na watu kadhaa aliowajua lakini hakumwona Mercy.

‘Labda ni kuchelewa tu,’ Simon aliwaza moyoni.

Related posts